" RC MRINDOKO AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI BILIONI 1.7 KWA WANANCHI WALIOPISHA ENEO LA UPANUZI WA CHUO CHA KILIMO SOKOINE (CAMPUS YA MIZENGO PINDA)

RC MRINDOKO AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI BILIONI 1.7 KWA WANANCHI WALIOPISHA ENEO LA UPANUZI WA CHUO CHA KILIMO SOKOINE (CAMPUS YA MIZENGO PINDA)

Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaMkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.7 kwa wananchi wa Kijiji cha Kibaoni, waliopisha eneo lenye ukubwa wa ekari 689.02 kwa ajili ya upanuzi wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA) – Campus ya Mizengo Pinda.Aidh hatua hiyo ni ushahidi wa dhamira ya serikali katika kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo, akiwapongeza wananchi kwa uzalendo wao na ushirikiano waliouonyesha. Ameongeza kuwa serikali itaendelea kusimamia haki za wananchi wote wanaopisha miradi ya kitaifa, sambamba na kuhakikisha fidia inatolewa kwa wakati na kwa uwazi.Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Godfrey Pinda, amesisitiza wananchi kutumia fidia hiyo kwa malengo yenye tija, akiwataka kuwa waangalifu dhidi ya watu wanaoweza kutumia nafasi hiyo kuwatapeli. Amesema serikali itaendelea kutoa elimu ya matumizi bora ya fedha za fidia ili wananchi waweze kujiletea maendeleo endelevu.Naye Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda, amewahimiza wananchi kutumia fedha hizo kwa busara na hekima, kwa kuzingatia mipango ya familia na mahitaji ya msingi yatakayoboresha maisha yao kwa muda mrefu. Amesema fedha hizo zitakuwa na manufaa makubwa endapo zitatumika kwa utulivu, umoja na maelewano katika jamii.Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wawakilishi wa wananchi na wakazi wa Kijiji cha Kibaoni, ambao walielezea furaha yao kwa hatua hiyo na kuahidi kutumia fidia waliyoipokea kwa njia yenye manufaa kwao na kwa vizazi vijavyoMkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, akizungumza.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post