Treni ya SGR iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea
Dodoma imepata ajali baada ya kuacha njia yake katika eneo la Ruvu.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema ajali ya treni
ya SGR iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma leo katika eneo
la Ruvu imesababishwa na hitilafu za kiuendeshaji.
TRC imesema uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo unaendelea, na hadi sasa hakuna
kifo kilichoripotiwa.




Post a Comment