" YANGA YAICHAPA AS FAR 1–0, YAENDELEA KUWIKA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

YANGA YAICHAPA AS FAR 1–0, YAENDELEA KUWIKA LIGI YA MABINGWA AFRIKA






Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wameibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya AS FAR Rabat katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika uliopigwa leo, Novemba 22, 2025, katika Dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Yanga SC walipata bao pekee la mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wao Prince Dube dakika ya 58, akimalizia kwa ustadi pasi ya kutengeneza nafasi iliyotolewa na Mudathir Yahya.

Kwa ushindi huo, Yanga SC wamefanikiwa kuvuna pointi tatu muhimu wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, na hivyo kujiweka kwenye mazingira mazuri katika harakati zao za kusaka nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo barani Afrika.


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
✉️ info@eastafricanspirits.com

Post a Comment

Previous Post Next Post