Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMbeyaWananchi wa Jiji la Mbeya, Novemba 18, 2025, wameandika historia mpya baada ya kufunguliwa kwa Home Tan Supermarket, moja ya supermarket kubwa na ya kisasa kufunguliwa katika eneo la Kabwe.Kwa muda mrefu wakazi wa Mbeya walikuwa wakitegemea huduma za aina hii katika mikoa mingine kama Dar es Salaam, jambo lililosababisha wengi kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huo na kujipatia bidhaa zenye ubora.Mapema asubuhi wananchi walifurika katika supermarket hiyo, wakivutiwa na bidhaa mbalimbali hasa za matumizi ya nyumbani, huku wengine wakifurahia punguzo maalum la bei lililotolewa kwa siku za uzinduzi ambalo litadumu kwa siku saba.Mmoja wa wananchi waliohudhuria hafla hiyo akiwemo Furaha Mhando, amesema kufunguliwa kwa supermarket hiyo ni neema kwa vijana kwani sasa wanaweza kujipatia ajira na kuachana na makundi yasiyofaa."Huduma hii iwe fursa kwa vijana kujipatia kipato kuliko kujihusisha na mambo yasiyofaa,” alisema Mhando.Kwa upande wake, Bi. Subira Mwakirembe amesema wakazi wa mkoa wa Mbeya wameipokea supermarket hiyo kwa furaha kubwa, hasa kutokana na ofa kabambe za bidhaa zilizonadiwa kwa punguzo maalum. “Tumefurahi kuona huduma kama hii hatimaye inafika Mbeya; ofa hizi za uzinduzi zimetunufaisha sana,” alisema Mwakirembe.Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Home Tan Supermarket, Elinihaki Richard Ngure, amesema supermarket hiyo imeanzishwa kwa ubunifu wa kipekee ili kusogeza huduma bora karibu zaidi na Wananchi."Tumeanza na punguzo la asilimia 20 kwa bidhaa nyingi kama sehemu ya shukrani kwa wananchi wa Mbeya, na tunawakaribisha wote waje kufurahia huduma bora na za kisasa,” alisema Ngure.Naye Bw. King Slee, mwekezaji kutoka China, amesema amefurahishwa na muitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa Mbeya na kusisitiza kuwa kampuni inapanga kusambaza huduma hizo katika mikoa mingine ikiwemo Iringa, Dodoma na Njombe ili kuongeza upatikanaji wa huduma bora na za uhakika.Hata hivyo Mgeni rasmi katika ufunguzi huo amekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamini Kuzaga.



































Post a Comment