Na Shinyanga RRHHOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo Novemba 21, 2025 imeungana na dunia kuadhimisha Siku ya Watoto Wanaozaliwa Njiti (World Prematurity Day), tukio ambalo limefanyika katika Idara ya Watoto Njiti (NICU) na limehudhuriwa na wazazi, wahudumu wa afya na viongozi wa hospitali.Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali, Dkt. Luzila John, ameipongeza Idara ya NICU kwa kuandaa siku hiyo muhimu ambayo imeendelea kuongeza uelewa wa jamii kuhusu changamoto na mahitaji ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.Amesema juhudi za watumishi wa NICU zimekuwa nguzo muhimu katika kuokoa maisha ya watoto wengi wanaohitaji uangalizi wa hali ya juu.Dkt. Luzila ametumia nafasi hiyo kuahidi kuwa hospitali itaendelea kuboresha huduma kwa kuongeza vifaa tiba katika kitengo hicho ili kuhakikisha watoto njiti wanapata matibabu ya kisasa na salama.Ameeleza kuwa uwekezaji wa vifaa hivyo ni hatua muhimu katika kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuimarisha huduma za mama na mtoto.Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwajali wagonjwa wote wanaohudumiwa hospitalini kwa kuwapa lugha nzuri, huduma yenye staha na uangalizi wa karibu.Amesema tabia na mwenendo wa watumishi vinachangia kwa kiasi kikubwa ustawi wa wagonjwa na kujenga imani ya wananchi kwa taasisi hiyo.Katika kuadhimisha siku hiyo, Idara ya NICU imetoa zawadi kwa akina mama wanaolea watoto njiti, ikiwa ni pamoja na nauli za kuwasaidia kurejea majumbani pamoja na taulo za watoto (pampers), kama ishara ya kuwafariji na kuwaunga mkono katika safari yao ya malezi.Maadhimisho hayo pia yamepambwa na hafla fupi ya kukata keki, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea hatua kubwa zinazopigwa katika utunzaji wa watoto njiti na kutambua kazi kubwa inayofanywa na watoa huduma katika kuokoa maisha ya watoto hao.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali, Dkt. Luzila John, akizungumza.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
✉️ info@eastafricanspirits.com





Post a Comment