" MARIDHIANO NA UADILIFU: TAMKO LA KIISLAMU LAWEKA MASHARTI YA KUDUMU KWA AMANI YA TAIFA

MARIDHIANO NA UADILIFU: TAMKO LA KIISLAMU LAWEKA MASHARTI YA KUDUMU KWA AMANI YA TAIFA



Katika tamko lao, Taasisi za Kiislamu zimeainisha msimamo wao thabiti kuhusu mchakato wa maridhiano ya kitaifa, wakisisitiza kwamba maridhiano hayo lazima yajikite kwenye uadilifu na dhamira njema, na siyo juu ya vuguvugu la muda mfupi au mashinikizo ya kisiasa.
Kauli hiyo waliitoa baada ya kukamilika kwa ibada ya itikafu,chini ya Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally.
Taasisi za kiislamu zilizokutana kwa ajili ya ibada ya itikafu katika Msikiti wa Mfalme Mohammed wa Sita, ambako pia ni makao makuu ya Bakwata jijini Dar es salaam ni Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), Umoja wa Madrassa Tanzania (Umata), Umoja wa Wahadhiri wa Kiislamu Tanzania (Tampro), Almaldi, Attaqwa Foundation, Al istiqama, Bohora na Taasisi ya Wanazuoni wa Kiislamu.
Taasisi nyingine ni Assalam Islamic Foundation, Al Amin Foundation, Ibn jazar ,Shia Ithnaasher, Baraza Kuu la Jumuiya za Kiislamu, Al Hikma Foundation, Tanzania Muslim Teachers’ Association (Tamta) Zahrawi Islamic Center, Shamsil Maarif, Maawal Islam Shamsil Hudda, Nurul Hudda na Munawwaral Madina. 
Viongozi hao wa dini wametamka wazi kwamba maridhiano kamwe yasiwe kichaka cha kuficha uhalifu. Wamependekeza uwepo wa uchunguzi wa kina wa kubaini watu binafsi, wanasiasa, na taasisi zilizochochea, kupanga, na kuratibu uhalifu uliotokea.
“Mchakato wa maridhiano, pamoja na umuhimu na ulazima wake, kamwe usituzibe macho tukashindwa kuun’goa mzizi wa fitina uliozaa maafa haya yaliyolitia doa Taifa letu,” ilisema sehemu ya tamko hilo.
Kwa kuunga mkono kuundwa kwa Tume Huru ya Uchunguzi, taasisi hizo zinaonyesha nia ya kuweka msingi wa amani ya kudumu, ambapo haki itasimama sawa bila kupindishwa, na kuhakikisha wale wasio na hatia wanalindwa. Kauli hii inaimarisha msimamo wa dini ya Kiislamu unaosisitiza umuhimu wa uadilifu kama msingi wa utulivu wa kijamii.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
✉️ info@eastafricanspirits.com

Post a Comment

Previous Post Next Post