" SMAUJATA NA POLISI SHINYANGA WATOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI MWAWAZA SEKONDARI

SMAUJATA NA POLISI SHINYANGA WATOA ELIMU YA KUPINGA UKATILI MWAWAZA SEKONDARI

Jumuiya ya kupinga ukatili nchini, SMAUJATA, inaendelea kuwa nguzo muhimu katika mapambano ya ukatili na ulinzi wa watoto nchini ambapo leo tarehe 21 Novemba 2025, Katibu wa Idara ya RME Taifa Ev. Vicent B. Kanyogoto akiambatana na SGT. Rose kutoka Dawati la Jinsia Shinyanga, wamefanya ziara ya kutoa elimu ya ukatili katika Shule ya Sekondari Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga.

Ziara hiyo imelenga kuwaandaa wanafunzi kuelekea likizo ya mwezi Desemba kwa kuwapatia elimu ya kujitambua, kujilinda na kutambua viashiria vya ukatili wanavyoweza kukutana navyo wakiwa nyumbani.

SGT. Rose kutoka Dawati la Jinsia Shinyanga amewaeleza wanafunzi kuhusu hatari wanazoweza kukumbana nazo wakati wa likizo, akisisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari mapema. Amefafanua masuala muhimu ambayo wanafunzi wanapaswa kuyazingatia, ikiwemo:

  • Kujikinga na ngono zembe wakiwa likizo

  • Kuepuka makundi hatarishi kama wavuta bangi

  • Kutoa taarifa mapema pale wanapoona viashiria vya ukatili, kuanzia kwa walimu hadi viongozi wa mitaa

  • Kuepuka kurekodi au kupakia video na maudhui yasiyofaa kwenye mitandao ya kijamii

  • Kujitambua na kujidhamini kama watoto wenye thamani katika taifa

Amesisitiza pia kuwa watoto ni sehemu muhimu ya rasilimali ya taifa, hivyo wana jukumu la kujilinda na kuthamini ndoto zao.


Katibu wa Idara ya Research, Monitoring and Evaluation (RME) Taifa, Ev. Vicent B. Kanyogoto, amewaelekeza wanafunzi juu ya umuhimu wa kujitambua ili waweze kutimiza malengo yao maishani. Amehimiza:

  • Kuweka na kutekeleza malengo yao ili baadaye wawe wazazi na viongozi bora

  • Kufanya tathmini ya maisha ya familia zao ili kupata nguvu ya kupambana na changamoto

  • Kujiamini na kufanya maamuzi sahihi bila kushawishiwa na makundi hatarishi

Mwisho wa ziara hiyo, Ev. Kanyogoto ameiomba Serikali kupitia wenyeviti wa mitaa kuwahamasisha wazazi kuhakikisha watoto hawatembei hovyo usiku au kujihusisha na michezo ya kamari kwenye mabanda, hususan kipindi cha likizo.

SMAUJATA inaendelea kuthibitisha kuwa ni shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii nchini, kwa kuendelea kuwalinda na kuwaongoza watoto kuelekea mustakabali bora.




 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
✉️ info@eastafricanspirits.com

1 Comments

  1. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

    dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete

Post a Comment

Previous Post Next Post