" WANAFUNZI 29,193 KUANZA MITIHANI YA UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI MKOANI SHINYANGA

WANAFUNZI 29,193 KUANZA MITIHANI YA UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI MKOANI SHINYANGA


Jumla ya wanafunzi 29,193 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Upimaji wa Kidato cha Pili mkoani Shinyanga kuanzia Novemba 10 hadi 19, katika shule mbalimbali za sekondari za mkoa huo.

Akitoa taarifa hiyo, Afisa Elimu wa Mkoa wa Shinyanga, Samson Hango, amesema kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 12,103, huku wasichana wakiwa 17,090. Aidha, amebainisha kuwa watahiniwa 42 ni wenye mahitaji maalumu.

Hango ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wote waliojiandikisha wanahudhuria mtihani kwa wakati, akisisitiza umuhimu wa kuwapa ushirikiano na motisha ili waweze kufanya vizuri.

“Ni muhimu wazazi na walezi wakawapa wanafunzi motisha na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kufanya mtihani huu kwa utulivu, kwani ni hatua muhimu katika maendeleo yao ya elimu,” amesema Hango.

Katika hatua nyingine, Afisa Elimu huyo ametoa onyo kali kwa walimu na watumishi wa sekta ya elimu watakaobainika kuhusika na vitendo vya udanganyifu au kuyumbisha mchakato wa mtihani huo, akieleza kuwa mtihani ni wa upimaji wa kawaida lakini una mchango mkubwa katika kupanga maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi.

Mtihani wa upimaji wa Kidato cha Pili hufanyika ili kupima maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi kabla ya kusonga mbele na hatua za juu za elimu ya sekondari.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA


Post a Comment

Previous Post Next Post