" WATANZANIA WASHAURIWA KUJIEPUSHA NA WAWEKA MAFUTA KWENYE NJIA YA UPONYAJI?

WATANZANIA WASHAURIWA KUJIEPUSHA NA WAWEKA MAFUTA KWENYE NJIA YA UPONYAJI?

Licha ya nia thabiti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuponya taifa na kuleta maridhiano ya kweli, wito unatolewa kwa Watanzania kujitathmini na kukemea baadhi ya watu na taasisi zinazodaiwa kuweka ‘mafuta kwenye moto’ na kuzuia safari ya umoja wa kitaifa.

Rais Samia alionyesha moyo wa unyenyekevu na huruma kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025, kwa kutoa pole za dhati kwa wale wote walioathirika.

"Nimehuzunishwa sana na tukio lile. Natoa pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu na jamaa. Tunaomba Mungu aziweke roho zao mahali pema. Kwa majeruhi, tunawaombea wapone haraka, na kwa waliopoteza mali, tunawaomba wawe na stahamala na uvumilivu,” alisema Rais Samia.

Katika mahojiano na wadau mbalimbali  baada ya hotuba ya Rais Samia yenyen lengo la uponyaji na kuzuka kwa kauli mbalimbali nchini kuhusu ni nani au nini kinakuwa kikwazo ya safari hiyo, wamnesema ni kibri na ubinafsi.

Mfanyabiashara wa  Tanga Bw. Rashid Mwinyi  "Demon (kikwazo) wetu mkubwa ubinafsi. Bila Amani Hakuna Maendeleo! Utulivu ndio Uzalendo wa Kweli."

Mch. Neema Mwasonga wa Mbeya anasema : "Kikwazo ni roho ya kutoamini katika taasisi zetu. Tunaona maoni mengi katika matandao kama 'ohh Tumeunda Tume Nyingi Sana Hazijawahi Kuja Na Majibu'. Si kweli majibu yapo ni lazima Watanzania waiunge mkono serikali kwa imani kuwa hekima na utulivu vipo kwa viongozi wetu, na tutafanikiwa."

Mkazi mmoja wa Dar es salaam Dkt. Imani Kileo  anasema : "Wale wanaokwamisha ni wanaochochea chuki kwa kutumia mitandao na wanaokataa kulegeza misimamo yao ya kisiasa na ya kiimani. Rais anataka maridhiano, lakini wengine wanatafuta 'Mbuzi wa Bwana Kheri' wa kulaumu badala ya kuvaa jezi moja ya TANZANIA."

Mjasirimali wa Arusha Bi. Stela Mushi  "Anasema kikwazo ni kushindwa kuona mbali. Vurugu zimerudisha nyuma biashara zetu. Bila Amani Hakuna Maendeleo! Tusiangalie tofauti zetu ndogo ndogo. Tuvuke hayo. Tufanye Kazi, Tukue Haraka!"

Kauli ya Rais Samia kuhusu msamaha na pole inaweka msingi wa kihisia na kimaadili kwa uponyaji. Hata hivyo, wajibu wa uponyaji wa taifa si wa Rais pekee, bali ni wa kila Mtanzania.

Kama inavyosisitizwa katika jumbe mbalimbali, siri ya kufika mbali haraka sio ngumu: ni kila Mtanzania kukubali kuwa Wote Pamoja, Kazi Iende Haraka! Tofauti zetu zikiwekwa kando, tunaweza kukabiliana na  shida yetu ya kutokuaminiana na urasimu.

Kwa kumuunga mkono kiongozi wetu kwa vitendo, na kufanyia kazi maelekezo yake, tunaweza kutimiza malengo ya taifa na kuhakikisha tunavuka salama. Umoja na mshikamano katika kujenga taifa letu ndio dira.


Post a Comment

Previous Post Next Post