AIC KAMBARAGE CHOIR WAGENI RASMI WA MKUTANO WA KRISMASI 2025 KAHAMA
Watumishi wa Bwana,
AIC Kambarage Choir inapenda kuwajulisha wapendwa wote kuwa, katika kipindi chote cha Sikukuu ya Krismasi kuanzia tarehe 23–25/12/2025, tutakuwa Kanisa la AIC Nyakato – Kahama kwa ajili ya kutoa huduma ya kuliinua na kulitukuza Jina Takatifu la Yesu Kristo kupitia nyimbo za sifa, shukrani na ibada.
Tunawaalika kwa moyo mkunjufu wakazi wote wa Kahama na maeneo ya jirani kujitokeza AIC Nyakato, ili kwa pamoja tumwinulie Kristo kwa kuyaimba matendo yake makuu, tukishuhudia upendo, neema na uwepo wa Mungu katika msimu huu wa Krismasi.
Hakika, Yesu atazaliwa mioyoni mwetu tunapokusanyika kumwabudu kwa roho na kweli.
Halleluyaaaa! 🙌🔥
📣 UKUMBUSHO MUHIMU
Tunawakumbusha wapendwa wote kuendelea:
✅ Kununua tisheti na sweta rasmi za USIKU WA SHUKURANI kama sehemu ya kuunga mkono maandalizi ya tukio
✅ Kujitokeza kama wadhamini—taasisi, kampuni na watu binafsi—kwa ajili ya kufanikisha Tamasha la USIKU WA SHUKURANI linalotarajiwa kufanyika Januari 30, 2026, katika Kanisa la AIC Kambarage, Mjini Shinyanga.
Ushiriki wako ni sehemu ya baraka tele, na mchango wako unagusa maisha ya wengi.
Karibu tushirikiane kumrudishia Bwana utukufu kwa vitendo!
📞 MAWASILIANO – MANUNUZI YA TISHETI & UDHAMINI
📱 +255 685 788 063 – AICT Kambarage Choir
📍 Wauzaji Shinyanga:
• Majengo & Mjini: Leonadia – +255 614 028 803
• Kambarage & Ndala: Abel – +255 628 495 081

Post a Comment