" Askofu Bagonza Ataja ‘Sumu’ Tano Zinazoua Maridhiano

Askofu Bagonza Ataja ‘Sumu’ Tano Zinazoua Maridhiano

 

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza.
Picha: Mtandao
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza, ametaja uwepo wa ‘sumu’ tano zinazoua maridhiano katika jamii, akiwataka Watanzania kujiepusha nazo ili kujenga amani ya kudumu.

Askofu Bagonza ameyasema hayo wakati wa ibada ya ubarikio wa wachungaji na wadiakonia iliyofanyika katika Dayosisi ya Karagwe, mkoani Kagera.

Akieleza sumu ya kwanza, amesema ni hila, akibainisha kuwa mara nyingi hufichwa kwa majina ya nia njema au maslahi mapana ya taifa. Aliwaasa watu kuacha hila wanapotafuta maridhiano ya kweli.

“Wakati mwingine, hila inapewa jina la nia njema au maslahi mapana ya taifa. Tujiepushe na hila kutafuta maridhiano,” alisema Askofu Bagonza.
Ametaja sumu ya pili kuwa ni kutafuta ushindi katika maridhiano, akionya kuwa kuweka mazingira ya mshindi na mshindwa huandaa migogoro na vurugu za baadaye.

Kwa upande wa sumu ya tatu, Askofu Bagonza amesema ni kukwepa ukweli, akisisitiza kuwa maridhiano ya kweli hupatikana pale ukweli unapowekwa wazi, hata kama unaumiza pande zote.

“Maridhiano yanapatikana endapo ukweli umeonekana hata kama unaumiza pande zote. Duniani kote, maridhiano hujengwa katika ukweli pasipo kulaumiana,” alifafanua.

Post a Comment

Previous Post Next Post