" CHADEMA YAKUSANYA MILIONI 14 NDANI YA SAA 24 KUMUUNGA MKONO TUNDU LISSU

CHADEMA YAKUSANYA MILIONI 14 NDANI YA SAA 24 KUMUUNGA MKONO TUNDU LISSU

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kukusanya jumla ya shilingi milioni 14 ndani ya saa 24 kupitia kampeni ya “Masaa 48 ya Kufunga Mwaka na Lissu”, ikiwa ni hatua ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Tundu Lissu, ambaye yupo kizuizini kwa zaidi ya miezi tisa.

Fedha hizo zimetolewa na Watanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi, kwa lengo la kusaidia mahitaji ya msingi ya Lissu kama vile chakula, usaidizi kwa familia yake, pamoja na kugharamia taratibu za kisheria zinazohusu kesi yake.

Kwa mujibu wa CHADEMA, mazingira ya maisha gerezani kwa Lissu yamekuwa magumu, hasa kwa kuwa huduma nyingi za kijamii na mawasiliano si rahisi kupatikana.

Chama hicho kimesema kuwa kampeni hiyo ni ishara ya mshikamano wa kweli kutoka kwa Watanzania, na ni uthibitisho wa heshima wanayoendelea kuwa nayo kwa Tundu Lissu kutokana na msimamo wake thabiti katika kusimamia haki, uwajibikaji na utawala wa sheria.

Aidha, CHADEMA imewahimiza Watanzania kuendelea kuonesha mshikamano wao kwa Lissu katika kipindi hiki kigumu, huku wakihamasishwa kufuatilia taarifa zaidi kupitia kurasa rasmi za chama hicho.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post