Na: Bernardo Costantine, Misalaba Media
Serikali kupitia Mkuu wa Mko wa Dar es salaam imesisitiza kuwa miili ya wagonjwa wanaofariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu hospitalini, itatolewa bila malipo na kwa haraka ili kuwawezesha ndugu na jamaa kufanya taratibu za mazishi bila kukutana na chagamoto yoyote wakati wa mazishi .
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini hapa ,akitanabaisha maboresho ya huduma za jamii jijini Dar es salaam na Tanzania Kwa ujumla.
Aidha amesema hatua hiyo inalenga kupunguza changamoto zinazowakumba wananchi katika kipindi cha majonzi, hususani wale wanaokosa uwezo wa kugharamia huduma mbalimbali baada ya kufiwa na wapendwa wao.
"Lengo ni kuhakikisha wananchi hawapati usumbufu wa ziada wanapokuwa katika kipindi kigumu cha kuondokewa na ndugu zao. Mwili unapaswa kutolewa mara moja ili taratibu za mazishi ziendelee,"
Amesema
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment