Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaMkuu wa ilaya ya musoma Mhe Juma Chikoka akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya elimu halmashauri ya Wilaya ya musoma amewataka wasiamamizi na mafundi wanaosimamia na kujenga majengo ya madarasa hasa katika shule mpya, ambapo miradi yote hii inatekelezwa kwa fedha ya serikali kuu kwaajili ya kusaidia na kupunguza umbali mlefu kwa wanafunzi hasa wanaoishi mbali na shule katika maeneo yao.Chikoka amepitia na kukagua majengo ya madarasa na ofisi katika shule mpya zinazojengwa na kuwataka mafundi na wasimamizi kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha ifikapo Jan.13,2026. Miradi hio ya elimu ipokee wanafunzi kwaajili ya kupata elimu.Nao baadhi ya wakazi na wanufaika wa mradi kijiji cha kabodi kata ya Nyamlandilila, wameishukuru serikali kwa kujenga shule na kukarabati baadhi ya madarasa kwani watoto walikua wakitembea umbali mlefu kuifuata elimu,"Kwakweli tunaishukuru serikali yetu pendwa kwaajili ya kujenga shule mpya ambazo zinaondoa adha ya watoto wetu kutafuta elimu kwani watoto wetu walipata changamoto kubwa kwa kutembea umbali mrefu kuzifikia shule, na wakati mwingine waliishia njiani na kukataa shule kwaajili ya mwendo, ila sasa shule hizi mpya zinapunguza hali hio." Alesema Mwananchi.Pia baadhi ya wazazi waliendelea kueleza changamoto ya walimu na kuomba baada ya shule hizo kukamilika wapate waalimu kwaajili ya kufundisha watoto wao.Katika hatua hio Mhe. Chikoka amewataka pia wazazi na walezi baada ya sikukuu kuisha kwa wale waliowasafirisha na kuwapeleka watoto kwa ndugu kula sikukuu, wawarejeshe mapema kwaajili ya kuendelea na masomo hasa katika kipindi cha mwanzo wa mwaka.
Mkuu wa ilaya ya musoma Mhe Juma Chikoka, akitoa maagizo.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment