Na Fabius Clavery, Misalaba Media-Kagera.Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Mhe. Zaituni Msofe, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kutumia mapato ya ndani, akisisitiza kuwa juhudi hizo zina mchango mkubwa katika kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.Mhe. Msofe ametoa pongezi hizo Desemba 23, 2025, wakati wa uzinduzi wa Wodi ya Wazazi (Mama na Mtoto) iliyojengwa katika Zahanati ya Songambele, wilayani Kyerwa. Amesema mradi huo ni sehemu ya usimamizi mzuri wa rasilimali na matumizi sahihi ya fedha za umma.Aidha, amepongeza uongozi wa Halmashauri hiyo unaoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Bahati Henerico, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, SACF James John, kwa kusimamia vyema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.Wodi hiyo imejengwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali, ikiwemo matumizi ya mapato ya ndani ya Halmashauri, fedha kutoka Serikali Kuu, mchango wa Shirika lisilo la Kiserikali la CBIDO, pamoja na michango ya wananchi, jambo lililoonesha mshikamano na ushirikishwaji wa jamii katika maendeleo yao.Mhe. Msofe amewahimiza wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo na kuitunza miundombinu hiyo ili iweze kutoa huduma bora na endelevu kwa akina mama na watoto.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Mhe. Zaituni Msofe, akizungumza.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment