" MKURUGENZI WA MGODI WA MAGESA GOLD MINE AWATAKIA WATANZANIA HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA

MKURUGENZI WA MGODI WA MAGESA GOLD MINE AWATAKIA WATANZANIA HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA

Mkurugenzi wa Mgodi wa Magesa Gold Mine, uliopo Nyamatagata, Mkoa wa Geita, amewatakia Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya, akiwatakia amani, afya njema na mafanikio katika shughuli zao za kila siku.

Ametoa salamu hizo wakati akizungumza na Misalaba Media ambapo amesema kuwa kipindi cha sikukuu ni muda wa kutafakari, kushukuru na kuimarisha mshikamano wa kitaifa, huku akiwahimiza Watanzania kuendelea kudumisha amani na kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya taifa.

Aidha, amewashukuru wafanyakazi wa mgodi huo pamoja na jamii inayouzunguka mgodi kwa ushirikiano mzuri, akiahidi kuendelea kushirikiana na serikali na wananchi katika kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Amehitimisha kwa kuwatakia Watanzania wote mwaka mpya wenye mafanikio, mshikamano na maendeleo endelevu.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post