" DCEA: VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA LAKINI WAKO HATARINI KUATHIRIWA NA MADAWA YA KULEVYA

DCEA: VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA LAKINI WAKO HATARINI KUATHIRIWA NA MADAWA YA KULEVYA

Na Fabius Clavery -Misalaba, Media Kagera.‎Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini (DCEA) imesema kuwa vijana ni nguvu kazi muhimu ya Taifa, lakini kwa sasa wako katika hatari kubwa ya kuathiriwa na matumizi ya madawa ya kulevya.OfKauli hiyo imetolewa na Dezdel Tumbu ofisa Mwandamizi Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa , Desemba 19 2025,wakati akizungumza na Misalaba Media katika Jukwaa la Uwekezaji Kagera lililofanyika katika Viwanja vya KCU, mjini Bukoba.‎Ofisa huyo amesema kuwa vijana ndio kundi kubwa linaloathirika na madawa ya kulevya, hali inayotokana na ukosefu wa elimu sahihi au kushawishiwa kujiingiza katika matumizi na biashara ya madawa hayo.‎Aidha, ameonya kuwa mtu yeyote atakayejihusisha kwa namna yoyote na madawa ya kulevya atachukuliwa hatua kali za kisheria kulingana na sheria za nchi.‎“Kundi kubwa linaloathiriwa na madawa ya kulevya ni vijana,Ndio maana tupo hapa katika Tamasha la Ijuka Omuka, kipindi ambacho wakazi wengi wanarejea nyumbani, ili kuwafikia wananchi wengi zaidi. Lakini pia niwaambie wananchi kuwa adhabu ya kukutwa na madawa ya kulevya ni kuanzia kifungo cha miaka 30 hadi kifungo cha maisha,” amesema afisa huyo.‎Mamlaka ya DCEA inashiriki katika Tamasha la Ijuka Omuka Linaloendelea Mkoani Kagera tangu Desemba 18 kwa lengo la kutoa elimu kwa vijana na wakazi wa Mkoa wa Kagera kuhusu madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya, pamoja na kuwahamasisha kujiepusha na vitendo hivyo.‎Kwa upande wake Rizick Massawe, mmoja wa vijana waliotembelea banda la DCEA katika tamasha hilo, ameiambia Misalaba Media kuwa amepata elimu ya kutosha kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya, na ameahidi kuwa balozi mzuri kwa vijana wengine mkoani Kagera.


Post a Comment

Previous Post Next Post