" George Simbachawene “Watoto Kuanza Kupatiwa Vitambulisho vya NIDA”

George Simbachawene “Watoto Kuanza Kupatiwa Vitambulisho vya NIDA”

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene amesema Serikali ipo katika maandalizi ya kusajili watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ili kuwapatia namba ya utambulisho wa kipekee (Jamii Namba) itakayotumika kuanzia kuzaliwa hadi mwisho wa maisha ya mtu.

Simbachawene ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua uzalishaji wa vitambulisho katika Kituo cha Kuchakata Taarifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambapo amesema zoezi hilo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Agosti 10, 2023, Usajili utaanza kwa watoto katika wilaya za Kilolo, Kusini Unguja na Runge utakao gharimu jumla ya shilingi bilioni 11.3

“Jamii namba itakayowatambua watoto ni jambo kubwa linalokuja Itapunguza malalamiko mengi kwa sababu mtu atatambulika tangu anapozaliwa,” amesema Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene.

Post a Comment

Previous Post Next Post