" UMMY NDERIANANGA ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA WENYE ULEMAVU

UMMY NDERIANANGA ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA WENYE ULEMAVU






Na. OWM SBU,Dodoma

‎Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Ummy Nderiananga, ameongoza kikao kazi maalumu cha Kitengo cha Wenye Ulemavu kilichofanyika katika Ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni Jijini Dodoma.

‎Serikali inaendelea kuweka mkazo katika kuwajengea uwezo Watu Wenye Ulemavu ili washiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii, kiuchumi na kimaamuzi.

‎Ameelekeza kuanzishwa kwa Kamati za Wenye Ulemavu kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa ili kutoa sauti na kushughulikia masuala yao kwa ufanisi.

‎Amesisitiza kuwa shughuli zote za Wizara, taasisi na mashirika yanayohusika na masuala ya Watu Wenye Ulemavu katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa zitambuliwe na Ofisi ya Waziri Mkuu, hususan Kitengo cha Wenye Ulemavu.

‎Aidha, amewakaribisha watumishi wa Kitengo cha Wenye Ulemavu waliohamia kutoka ofisi iliyokuwa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.





Post a Comment

Previous Post Next Post