Na Mapuli Kitina MisalabaJeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo kuelekea sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya, kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Janeth Magomi amesema Jeshi hilo limeongeza doria na ulinzi katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo nyumba za ibada, maeneo ya starehe, barabarani pamoja na maeneo mengine ya kijamii ili kuzuia na kutanzua vitendo vya kihalifu.
SACP Magomi ametoa wito kwa madereva wote kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuwa waangalifu wakati wote wanapotumia vyombo vya moto na kuepuka mwendo wa kasi unaoweza kusababisha ajali.
Pia amewakumbusha wazazi na walezi kuendelea kuwajibika katika ulinzi na usimamizi wa watoto wao, hususan katika maeneo ya barabarani na sehemu za michezo, ili kuepusha ajali na matukio yanayoweza kuhatarisha usalama wao.
Kwa wananchi wanaotarajia kusafiri au kwenda kusherehekea sikukuu nje ya makazi yao, SACP Magomi amewasisitiza kuchukua tahadhari ikiwemo kufunga nyumba vizuri kabla ya kuondoka ili kuepuka matukio ya uhalifu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawatakia wananchi wote sherehe njema za Krismas na Mwaka Mpya, likisisitiza kuwa litaendelea kulinda amani na usalama katika kipindi chote cha sikukuu.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment