Na Mapuli Kitina MisalabaKaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Kambira Mtebe ametoa salamu za heri ya Krismas na Mwaka Mpya kwa wananchi wote Manispaa ya Shinyanga na maeneo jirani ya Tinde, Didia na Iselamagazi.
Katika salamu hizo, Kaimu Mkurugenzi amewashukuru wateja wa SHUWASA kwa ushirikiano wao, uvumilivu na uaminifu waliouonesha katika kipindi chote cha mwaka, hali iliyosaidia mamlaka hiyo kuendelea kuboresha huduma za maji safi na salama.
Aidha, amewahimiza wananchi wote kusherehekea sikukuu hizo kwa amani, upendo na mshikamano, huku akiwasisitiza kuendelea kulinda miundombinu ya maji na kuzingatia usafi wa mazingira katika kipindi cha sikukuu.
SHUWASA inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuboresha huduma za majisafi na usafi wa mazingira kwa manufaa ya wananchi wa Manispaa ya Shinyanga na maeneo ya Tinde, Didia na Iselemagazi🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment