Na Mapuli Kitina Misalaba
Katika kikao cha wanakikundi wa Shinyanga Chapa ya Ng’ombe, mmoja wa walezi wa kikundi, ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Wilaya ya Shinyanga, Hasna Maige, ametumia fursa hiyo kutoa elimu muhimu kuhusu masuala ya ukatili.
Hasna Maige amesisitiza kwamba wanakikundi wanapaswa kuendelea kuwa mabalozi wa amani na kuepuka vitendo vyote vya ukatili, ikiwemo unyanyasaji wa wanachama na kunyimana haki ndani ya kikundi.
Amesema ushirikiano, heshima na mshikamano kati ya wanakikundi ni nguzo muhimu ya maendeleo ya kikundi na jamii kwa ujumla.
Aidha, Hasna Maige amewahimiza wanakikundi kukemea vitendo vya ukatili vinavyojitokeza katika jamii na kutoa taarifa mara moja kwa viongozi husika pindi vitendo hivyo vinapotokea. Taarifa hizo zinaweza kuwasilishwa kwa:
-
Viongozi wa kikundi, iongozi wa serikali za mitaa, Viongozi wa dini, Viongozi wa SMAUJATA na Kupitia namba ya bure 116
Hatua hizi, amesema Hasna, ni muhimu ili serikali ichukue hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika wanaojihusisha na ukatili, na kuhakikisha jamii inabaki salama, mshikamano unadumishwa, na haki za kila mmoja zinaheshimiwa.
Mchango wa Hasna Maige unathibitisha umuhimu wa elimisho na uelewa kama njia ya kuondoa vitendo vya ukatili na kuimarisha mshikamano katika wanakikundi na jamii kwa ujumla ambapo elimu hiyo analenga kuhakikisha wanakikundi wanakuwa walinzi wa amani, wakiendelea kushirikiana na kuepuka migogoro au vitendo vya kibinafsi vinavyoathiri mshikamano wa kikundi.
Katibu wa Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Wilaya ya Shinyanga, Hasna Maige, akizungumza.









































Post a Comment