Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo akizungumza.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Pendo Sawa akizungumza.
Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Mazingira ya kisiasa ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga yamepata sura mpya baada ya Baraza la Madiwani kumchagua Diwani wa Kata ya Mjini, Salum Kitumbo, kuwa Meya mpya wa Manispaa, huku Diwani wa Ndembezi, Pendo Sawa, akitangazwa Naibu Meya.
Uchaguzi huo, uliofanyika leo Desemba 4, 2025, umeonyesha umoja na mshikamano wa kisiasa baada ya wagombea wote wawili kuibuka na ushindi wa kura 23 za ndiyo, sawa na asilimia 100 ya wajumbe waliohudhuria.
Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, ameusimamia mchakato huo kwa mujibu wa sheria, na kutangaza matokeo hayo kwa kauli iliyoacha wazi msimamo wa baraza hilo katika kujenga kasi mpya ya maendeleo.
“Kwa mamlaka niliyopewa, natamka rasmi kwamba Salum Kitumbo ndiye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga na Pendo Sawa kuwa Naibu Meya,” amesema Kitinga mara baada ya kuhesabu kura.
Kitumbo, ambaye amekuwa akitambulika kutokana na msimamo wake mkali kwenye hoja za maendeleo na uwajibikaji, sasa anakabidhiwa jukumu la kusimamia dira ya Manispaa katika kipindi ambacho wananchi wanahitaji matokeo ya harakahasa katika miundombinu, usafi, na uchumi wa mtaa.
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment