" BARAZA LA MADIWANI JIJINI ARUSHA LAZINDULIWA.

BARAZA LA MADIWANI JIJINI ARUSHA LAZINDULIWA.


Na, Egidia Vedasto, 
Misalaba Media, Arusha. 

Mkutano wa kwanza wa baraza la madiwani halmsahauri ya Jiji la Arusha umezinduliwa rasmi na kushuhudiwa na wananchi wakati  wakiapa kiapo cha uaminifu tayari kwa kuanza shughuli zao za kuwatumikia wananchi katika kata zao. 

Jumla ya madiwani 25 waliochaguliwa na madiwani 09 wa viti maalum kutoka kata 25 za jiji la Arusha wameapa mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Boniface Semroki kama ishara ya kuanza majukumu yao. 


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya  Katibu tawala wa wilaya ya Arusha mapema leo  Jacob Rombo amewapongeza madiwani wote kwa kuaminiwa na kuchaguliwa. 

Amesema kwa kipindi chote ambacho madiwani wamekuwa nje Mkurugenzi wa jiji la Arusha John Kayombo pamoja na wakuu wa idara wamehakikisha wanawatumikia wananchi ipasavyo kwa kata zote.


Hata hivyo katika mkutano huo Maxmillian Iranqhe ameibuka kidedea kwa nafasi ya Meya wa Jiji la Arusha kwa kura za ndio 33 kati ya kura 34, sambamba na Naibu meya Julius Medeiye aliyeibuka na ushindi wa kura 31 za ndio kati ya kura 34.

Baada ya Mstahiki Meya Maxmillian Iranqhe kuapishwa amefungua baraza na kusema kuwa katika baraza hilo jipya wataanzia pale walipoishia katika baraza lililopita ambapo suala la matengenezo ya barabara litapewa kipaumbele. 

"Jiji letu linakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao laki sita kumi na saba elfu, kati yao vijana wakiwa ni asilimia 60 ya watu wote. Ndugu zangu katika baraza hili tuhakikishe tunaweka mazingira bora na rafiki kwa vijana ili wapate fulsa ya kujikwamua na umaskini"amesema Iranqhe.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post