" MFUMO WA ELIMU TANZANIA

MFUMO WA ELIMU TANZANIA

MFUMO WA ELIMU TANZANIA:

* Wanafunzi wengi,ubora mdogo.

* Tatizo liko wapi?

Na: Mbeki Mbeki 

Kagera.

Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye upatikanaji wa elimu tangu uhuru mwaka1961,hasa katika kuandikisha wanafunzi wengi shuleni.

Hata hivyo,takwimu za ufaulu na ujuzi halisi kwa wahitimu zinaonyesha taswira tofauti:Wanafunzi ni wengi ,lakini elimu bora ni ndogo.

Wachambuzi wa elimu wanasema kuzorota kwa ubora kumeanza kuonekana zaidi baada ya mwaka 1985 ,kipindi ambacho idadi ya shule iliongezeka kwa kasi bila kuendana na uwekezaji wa kutosha kwenye raslimali za ufundishaji.

Miongoni mwa changamoto kubwa ni mitaala isiyolenga ujuzi wa vitendo,inayowapa wanafunzi maarifa ya kukariri kuliko kutatua matatizo.

" mfumo wetu ni wakufundisha mitihani,si kufundisha fikra"anasema mtaalamu wa sera za elimu Dkt.J.Mhando ,katika mahojiano ya hivi karibuni.

Pia,uhaba wa walimu wenye sifa na motisha duni kazini umeendelea kuwa kikwazo.

Uwiano wa kitaifa wa walimu kwa wanafunzi bado uko chini ya kiwango kinachoshauriwa na UNESCO ,huku baadhi ya shule zikiripoti kuwa na wanafunzi zaidi ya 90 darasani.

Miundo mbinu ya shule nayo inatajwa kuathiri moja kwa moja uelewa.

Shule nyingi hazina maabara ,maktaba  wala vifaa vya TEHAMA vinavyoweza kusaidia ujifunzaji wa kisasa.

Katika ziara yake ya mwaka huu ,mdhibiti wa ubora wa shule kanda ya mashariki Bi.R. Kagashe ,alisema baadhi ya maabara zinazotumika ni" Vyumba vya kawaida vilivyopewa jina la maabara".

Kwaupande mwingine,bajeti ya elimu imeendelea kuegemea zaidi kwenye usimamizi wa mitihani kuliko kuboresha ufundishaji.

 Hali ya kiuchumi ya familia nayo inaongeza changamoto,kwani wanafunzi wengi wanakosa vifaa vya ziada vya kujifunzia,lishebora na mazingira tulivu ya kusoma.

Licha ya changamoto hizo,wadau wa elimu wanaiona fursa kwenye mageuzi mapya iwapo aerikali itaweka kipaumbele kwenye:

* Utafiti wa kina kabla ya kubadili mitaala.

* Kuongeza ajira na maslahi ya walimu.

* Uwekezaji kwenye teknolojia ya elimu.

* Nakuimarisha elimu ya vitendo na ubunifu.

Aidha,Elimu ya Tanzania haikosi wanafunzi ,inakosa ubora unaojenga wanafunzi kwa ubunifu ,wenye ujuzi,na ushindani kwenye soko la ajira.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post