Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, amelaani vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa dini kutumia mamlaka na ushawishi wao kwa waumini kama kisingizio cha kuhalalisha migogoro na migawanyiko ndani ya mataifa yao.
Leo, ambaye ni Papa wa kwanza kutoka nchini Marekani, ameyasema hayo kupitia ujumbe wa kurasa nne uliotolewa kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani ya Kanisa Katoliki, yanayolenga kusisitiza umuhimu wa kulinda, kuimarisha na kudumisha amani katika jamii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 18, 2025, Papa Leo XIV amesema kumekuwapo na baadhi ya viongozi wa dini wanaotumia sera za uzalendo kama nyenzo ya kupandikiza chuki miongoni mwa waumini, kitendo ambacho amekitaja kuwa ni kufuru au dhambi kubwa inayomdharau na kumtukana Mungu.
“Kwa bahati mbaya, imekuwa jambo la kawaida zaidi kuivuta lugha ya imani katika vita vya kisiasa, kubariki utaifa, na kuhalalisha vurugu pamoja na mapambano ya silaha kwa jina la dini,” amesema Papa.
Amesema waumini wanapaswa kujifunza kukanusha kikamilifu mafundisho na maelekezo yote yanayotolewa na viongozi wa dini wenye mienendo hiyo, ili kuondoa uwezekano wa kuzuka kwa migogoro ndani ya taifa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment