" Rais Donald Trump Awafungulia Kesi Rasmi BBC ya Kumdhalilisha, Adai Mabilioni

Rais Donald Trump Awafungulia Kesi Rasmi BBC ya Kumdhalilisha, Adai Mabilioni

 

Rais Donald Trump wa Marekani amefungua kesi rasmi ya Kisheria dhidi ya Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, akidai kudhalilishwa (defamation) kutokana na uhariri wa hotuba yake ya Januari 6, 2021, ambao ulionekana kuwashawishi wafuasi wake kuvamia Jengo la Bunge Capitol ya Marekani.

Kesi hii inafungua kipande kipya cha Kimataifa katika mapambano ya Trump dhidi ya Vyombo vya habari anavyodhani vinazungumzia vibaya tena kwa njia isiyo ya haki.

Rais Trump anataka Dola Bilioni 5 za Marekani kama fidia kwa kila hoja mbili za kesi hiyo. Anadai kuwa BBC, Shirika la Umma la Uingereza, limchanganua sehemu za hotuba yake, ikiwemo sehemu moja ambapo aliwahi kuwataka wafuasi wake wapelekwe Capitol na nyingine ambapo alisema “fight like hell” (piganeni hadi mwisho), huku likiacha sehemu muhimu ambapo aliahidi Maandamano ya amani.

Hata hivyo, BBC imeomba radhi kwa Trump, ikikubali kosa la maamuzi na ikikiri kwamba uhariri huo ulitengeneza dhana isiyo sahihi kwamba Trump alikuwa ametoa wito wa vurugu. Shirika hilo limeeleza pia kuwa hakuna msingi wa Kisheria wa kesi hii, jambo linaloongeza changamoto kwa Trump.

Aidha, BBC inafadhiliwa kupitia leseni ya lazima ya televisheni kwa watazamaji wote nchini Uingereza, jambo ambalo Wanasheria wanasema linaweza kufanya malipo yoyote kwa Trump kuwa tatizo la kisiasa.

Kesi hii inachukuliwa kuwa sehemu ya juhudi za Trump za Kimataifa za kulinda jina lake na kupinga ripoti za Vyombo vya habari anavyodhani siyo sahihi, na inaweza kuwa changamoto kubwa Kisheria, kwani sheria za kudhalilisha Uingereza ziko tofauti na zile za Marekani, hasa kuhusu wigo wa uhuru wa Vyombo vya habari.

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post