" RC ARUSHA CPA MAKALLA AWAFUNDA MADIWANI JIJI LA ARUSHA.

RC ARUSHA CPA MAKALLA AWAFUNDA MADIWANI JIJI LA ARUSHA.


Na Egidia Vedasto, 

Misalaba Media. 

Baraza la madiwani Jijini Arusha limeaswa kukaa mguu sawa kuhakikisha linaleta mapinduzi makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu, usafi ukusanyaji mapato na mambo mengine kedekede. 

Akizungumza na baraza la madiwani la halmashauri ya jiji la Arusha, Mkuu wa mkoa Arusha CPA Amos Makalla amelitaka baraza hilo kukaa mguu sawa kuhakikisha wanabadilisha hali ya uchumi ya sasa na kuipandisha zaidi, sambamba na kufanya mandhari ya jiji kuvutia zaidi hatua itakayosaidia kuvutia zaidi wageni. 

Aidha amewataka kuiga mfano bora wa Majiji yaliyofanikiwa. Amesisitiza wasisubiri kusukumwa bali wajitume kuharakisha maendeleo kama walivyoahidi kipindi cha kampeni. 

Katika namna hiyo hiyo CPA Makalla ameonyesha mashaka ya kiwango cha utendaji kazi ukilinganisha na nafasi zao katika jamii. 

"Mliomba kazi wenyewe watendeeni wananchi wenu kama mlivyoahidi, mmebeba maono na ilani. Wananchi wanahitaji mabadiliko chanya na sio maneno matupu" Makalla amesema.


Vile vile amesisitiza suala mikopo ambalo limekuwa mwiba na kujawa na sintofahamu hiyo yote ikitokana na ukosefu wa taarifa na uwazi kuhusu mikopo hiyo. 

CPA Makalla ameshauri vikundi vyote vya vijana vitakavyopewa mikopo vitambulike na kuwekwa wazi, ili kuweka vizuri kumbukumbu na ushuhuda wa wanufaika. hatua hiyo itaondoa maswali na wasiwasi kuhusu po lakini yaarifa na uwazi namna ya watu kikopeshwa hakuna, nimeelekeza vijana wakipewa mikopo waitwe wapewe hadharani na vikundi vijulikane isipofanyika hiyo hawawezi kukubaliana nanyi. 

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Lemara Matuyan Laizer ameahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla. 

"Katika kipindi cha kampeni niliahidi kushughulikia changamoto za miundombinu ya barabara, usafi wa mazingira pamoja na kuhakikisha vijana wanapata mikopo ya halmashauri kama inavyoelekezwa. Naomba Mungu anisaidie niweze kutimiza ahadi yangu kwa wananchi" amesema Laizer. 

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post