
Rushwa imetajwa kuwa ni janga kubwa linaloharibu kwa kiwan go kikubwa mfumo mzima wa utoaji haki, hivyo kuhatarisha misingi ya haki, uwajibikaji na utawala bora.
Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 23, 2025 na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Uchumi wa Madini na Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (Local content & CSR), Terrence Ngole, ambaye amemwakirisha Katibu Mkuu Wizara ya Madini wakati akifungua mafunzo maalumu kwa Menejimenti ya Wizara ya Madini yanayolenga kujadili madhara ya rushwa pamoja na namna ambavyo rushwa inavyodhoofisha mfumo wa haki katika taasisi za umma.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Ngole amesema kuwa rushwa huathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa majukumu ya Serikali, hususan katika sekta nyeti kama utoaji wa haki, ambapo vitendo vya rushwa husababisha kukosekana kwa usawa, upendeleo na kupungua kwa imani ya wananchi kwa taasisi za umma.
“Rushwa ni adui mkubwa wa haki. Inapopenya katika mifumo ya utoaji haki, husababisha haki kununuliwa, sheria kupindishwa na wananchi kukosa imani na taasisi zilizoundwa kuwalinda,” amesema Ngole.
Ameongeza kuwa sekta ya madini, kama zilivyo sekta nyingine, inahitaji uadilifu wa hali ya juu kutoka kwa watumishi wake ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha Watanzania kwa haki na usawa, bila kuathiriwa na vitendo vya rushwa.
Katika mafunzo hayo, Menejimenti ya Wizara ya Madini pia imepata fursa ya kupitishwa juu ya maadili ya utumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na wajibu wa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya kazi, pamoja na umuhimu wa uwazi, uwajibikaji na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu Fatma Senkoro amesisitiza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha maadili, kupambana na rushwa na kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya haki na maslahi mapana ya taifa.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza uelewa wa viongozi wa wizara juu ya athari za rushwa na kuchochea mabadiliko chanya ya mwenendo katika utumishi wa umma, hususan katika kusimamia na kuendeleza sekta ya madini kwa manufaa ya Watanzania wote
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment