Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameuzindua rasmi Mji wa Dkt. Hussein Mwinyi uliopo Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi, na kuutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kuendelea kujikita katika utekelezaji wa miradi mikubwa yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 23 Disemba 2025, wakati wa uzinduzi wa mji huo wa kisasa, tukio lililofanyika ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema mifuko ya hifadhi ya jamii imekuwa chachu ya maendeleo katika nchi nyingi duniani, na kuipongeza ZSSF kwa kuanza vema utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa maendeleo, hususan katika ujenzi wa makazi ya kisasa na ya gharama nafuu.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameishauri ZSSF kujikita zaidi katika uwekezaji wa miradi mikubwa ikiwemo miradi ya nishati ya umeme, baada ya kufanya vizuri katika ujenzi wa masoko, vituo vya mabasi na nyumba za makaazi.
Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na miji mipya ya kisasa yenye haiba na ubora, ili wananchi waishi katika makaazi bora na mazingira salama. Ameongeza kuwa bado wananchi wengi wanaishi katika makaazi duni na mitaa isiyopimwa, hali inayosababisha changamoto za kimazingira na kupanga miji, na hivyo kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo.
Halikadhalika, uzinduzi wa Mji huo umeenda sambamba na uzinduzi wa nyumba za gharama nafuu pamoja na uzinduzi wa msikiti mpya uliojengwa katika eneo hilo, Masjid Balad Salaam.
Rais Dkt. Mwinyi amewataka ZSSF na wakaazi wa Mji wa Dkt. Hussein Mwinyi kuzitunza nyumba hizo kwa kushirikiana, ili ziendelee kuwa na haiba na ubora kwa muda mrefu.
Vilevile, Rais Dkt. Mwinyi ameridhia ombi la ZSSF la kupatiwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali Kisakasaka, na kuiagiza Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kuipatia taasisi hiyo eneo la ardhi kwa ajili ya ujenzi huo, huku akisisitiza kuwa ofisi zitakazojengwa ziwe bora na za mfano.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment