Picha zinazoonesha ushirikiano wa karibu kati ya wachochezi wa vurugu za Oktoba 29 na shirika kubwa la kimataifa la habari, CNN zimeendelea kuvuja huku watumiaji wa mitandao wakielezea ushirikiano huo haramu ukiwa ni sehemu ya "mradi" mpana unaolenga kuchafua taswira ya Tanzania na kuhamasisha vurugu ili kufikia lengo la kuangusha Serikali iliyopo madarakani.
Miongoni mwa picha hizo ni hii inayomuonesha Maria Sarungi akizungumza na mwandishi wa CNN, Mwandishi Larry Madowo raia wa Kenya ambaye aliandika makala yenye uwongo mkubwa ikiwamo kuwapo kwa kaburi la jumla pale kwa Kondo akidai ni picha za setelaiti.
Hata hivyo, wanamtandao wanahoji kuwa Chadema pamoja na wanaharakati wao hawajaenda kuonesha makaburi hayo yanayotajwa na Satellite "fake" ya CNN.
Imeelezwa katika mitandao kuwa Maria Sarungi ndiye aliyempatia malipo mwandishi huyo kwa kazi ya kuufanya uchafuzi ndani ya CNN dhidi ya Tanzania.
Mwandishi huyo wa CNN alijaribu kutumia ushawishi wake kuaminisha umma kwamba shirika hilo lilikuwa na picha za satelaiti zinazothibitisha uwepo wa makaburi hayo.
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment