
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya wanaume ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) uliochezwa leo, Desemba 30, 2025, nchini Morocco.
Licha ya matoke hayo, Taifa Stars imefuzu hatua ya mtoano baada ya wakifikisha pointi 2 na kushika nafasi ya tatu katika kundi C.
Hali hiyo imeipa Tanzania nafasi ya kuingia katika ushindani wa kuwania kufuzu kama moja ya timu nne bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu katika makundini.
Katika kundi C Nigeria wamemaliza wakiwa na pointi 9 , Tunisia wakiwa na pointi 6, huku Uganda wakiwa na pointi 1.
Katika mchezo wa leo, Tunisia walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 42 kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na Ismaël Gharbi.
Tanzania walipata bao la kusawazisha dakika ya 48 kupitia Feisal Salum Abdallah, maarufu kama Fei Toto, aliyefunga kwa shuti kali nje ya eneo la mita 18 na kumshinda kipa wa Tunisia.
January 4, 2025 Tanzania wataminyana na Wenyeji wa AFCON 2025 Morocco katika hatua ya mtoano.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment