" Taifa Stars Leo Kuchagua Kuendelea na AFCON Aula

Taifa Stars Leo Kuchagua Kuendelea na AFCON Aula

 

Taifa Stars inakabiliwa na mtihani mzito wa dakika 90 usiku wa leo itakaposhuka dimbani kuikabili Tunisia katika mchezo wa uhai na kifo wa AFCON 2025 Matarajio ya kusalia Morocco bado yapo lakini yanategemea jambo moja tu ushindi.

Hakuna hesabu wala nafasi ya makosa Matokeo yoyote tofauti na ushindi yataimaliza safari ya Tanzania katika mashindano haya na kuifanya iungane na Zambia,Botswana,Gabon na Guinea ya Ikweta ambazo tayari zimeaga mapema.

Ni mechi inayohitaji nidhamu umoja na mapambano ya hali ya juu kutoka kwa kila mchezaji Macho ya Watanzania yapo kwa Taifa Stars wakisubiri kuona kama ndoto ya kuendelea mbele itaendelea kuishi au itafikia tamati usiku wa leo..

 

Post a Comment

Previous Post Next Post