
NA DENIS MLOWE ,IRINGA
BONANZA la Ngajilo limeendelea kuvuta hisia za wakazi wa mkoa wa Iringa na wilaya za jirani kutokana na kuwa na michezo mbalimbali na kufanyika kwa mafanikio makubwa na kushirikisha makundi mbalimbali ya wananchi.
Tukio hilo, ambalo limeandaliwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mheshimiwa Fadhil Ngajilo, limepongezwa na viongozi, wadau wa michezo na wananchi waliohudhuria kwa wiki kila siku tangu Disemba 27 na litahitimika disemba 31.
Akizungumza katika bonanza hilo, Andrea Chiniko alieleza kuwa mchango wa Mbunge Ngajilo katika kuinua michezo ni wa kuigwa na unaonyesha dhamira yake ya kuwa karibu na vijana, wazee na watoto.
“Mheshimiwa Ngajilo ameonyesha mfano mzuri. Michezo ni ajira, ni afya, na ni umoja. Tunampongeza kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwa vijana,” alisema Chiniko.
Kwa upande wake, Vicente Ngailo alisema kuwa bonanza hilo limeleta hamasa mpya katika jamii, hususan kwa vijana ambao wamepata nafasi ya kuonesha vipaji vyao.
“Tumeshuhudia vipaji ambavyo vikipelekwa mbele vitaweza kutangaza taifa letu. Hili bonanza ni mwanzo mzuri, na tunamshukuru sana mbunge kwa moyo huu,” alisema Ngailo.
Mwanaharakati wa michezo, Madope Juma, alisifu maandalizi na ushiriki mkubwa wa wananchi, akiongeza kuwa tukio hilo limeimarisha umoja na mshikamano.
“Hatujaona bonanza kubwa la aina hii kwa muda mrefu. Mbunge ametengeneza jukwaa muhimu kwa vijana. Hili ni jambo la kupongezwa,” alisema Juma.
Naye Mwanaidi Hasan, mmoja wa wanawake walioshiriki katika shughuli za bonanza hilo, alieleza kufurahishwa na namna tukio hilo lilivyozingatia usawa wa kijinsia.
“Ni jambo jema kuona wanawake tunashirikishwa kikamilifu. Tunampongeza mheshimiwa mbunge kwa kutambua nafasi ya wanawake katika michezo na maendeleo kwa ujumla,” alisema Mwanaidi.
Bonanza la Ngajilo limeendelea kuwa kivutio katika eneo hilo, likichukuliwa kama ishara ya ushirikiano kati ya uongozi wa jimbo na wananchi katika kuhamasisha michezo, afya na maendeleo ya jamii.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment