Tunapoelekea mwaka 2030, Tanzania inatarajiwa kushuhudia mapinduzi makubwa ya kiuchumi ambayo msingi wake umewekwa katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ramani hii ya mafanikio haitegemei bahati, bali inategemea kukamilika kwa miradi ya kimkakati ambayo kwa sasa inatoa jasho na rasilimali nyingi za taifa. Ikiwa amani itadumu na mipango ya sasa ikatekelezwa bila kuingiliwa na vurugu za kisiasa, ifikapo mwaka 2030 maisha ya kijana wa Kitanzania yatakuwa na sura mpya kabisa.
Kukamilika kwa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa na ununuzi wa meli tano kubwa za uvuvi ni mwanzo wa safari. Ifikapo mwaka 2030, mnyororo wa thamani wa sekta ya uvuvi unatarajiwa kuwa na viwanda vya uchakataji samaki kando kando ya mwambao wa bahari ya Hindi na maziwa makuu.
Hii inamaanisha kuwa kijana wa mwaka 2030 hatakuwa anatafuta kazi ya ukarani tu, bali atakuwa mmiliki wa viwanda vidogo vya vifungashio, mtoa huduma za usafirishaji (logistics), na mtaalamu wa teknolojia ya kisasa ya uvuvi.
Bandari ya Kilwa pekee inategemewa kuchochea ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa watu zaidi ya 30,000, likiwa ni kundi kubwa la vijana.
Gridi ya Taifa ya Maji na kukamilika kwa miradi mikubwa ya umeme kama Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kutaifanya Tanzania kuwa na nishati ya uhakika na ya bei nafuu.
Mwaka 2030 unatarajiwa kuwa mwaka ambao kijana wa vijijini anaweza kuanzisha karakana ya kulehemu, kiwanda cha kusaga nafaka, au biashara ya saluni bila hofu ya kukatika kwa umeme au ukosefu wa maji safi. Uhakika wa huduma hizi utapunguza gharama za uendeshaji biashara (Cost of Doing Business), jambo ambalo litaongeza faida kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) na kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja.
Barabara kuu kama ile ya Marendego – Lindi na uboresha wa reli ya kisasa (SGR) vinaunganisha Tanzania na masoko ya nchi jirani kama Zambia, DRC, na Malawi. Ifikapo mwaka 2030, kijana wa Tanzania atakuwa na uwezo wa kusafirisha bidhaa zake kutoka viwanda vya ndani kwenda nchi yoyote ya jirani kwa gharama nafuu na muda mfupi. Hii inafungua fursa ya "Cross-border Trade" ambapo vijana watakuwa mawakala wa biashara za kimataifa, wakitumia bandari zetu zilizoboreshwa kama lango kuu la biashara barani Afrika.
Ramani hii ya mafanikio inaweza kutimia tu ikiwa kila tone la rasilimali litatumika kwa maendeleo badala ya kurudia michakato ya kisiasa isiyo na tija.
Mwaka 2030 utakuwa ni mwaka wa mavuno kwa wale waliojituliza na kuwekeza nguvu zao kwenye miradi na ubunifu badala ya kufuata kelele za wachochezi. Rais Dkt. Samia ameshaonesha njia; ni jukumu la kila kijana mzalendo kulinda amani ya sasa ili kuhakikisha kuwa safari hii ya kuelekea 2030 haikwami njiani. Tanzania ya kesho ni ya wale wanaoijenga leo kwa mikono yao na akili zao.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment