" Tanzia: Aliyewahi Kuwa Bingwa wa Disco Tanzania Afariki Dunia

Tanzia: Aliyewahi Kuwa Bingwa wa Disco Tanzania Afariki Dunia

 

Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa bingwa wa Taifa wa Club Raha Leo Show na mcheza disco maarufu nchini Tanzania, Savy Pops amefariki dunia.

Savy Pops ambaye jina lake halisi ni Francis Exaviery Ling’wentu amefariki leo Desemba 18, 2025 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kaka wa marehemu, Symphorian Ling’wentu (Muhenga Gablama) amethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii huyo.

Amesema ndugu yao amefariki saa 2 asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kansa.

Amesema mwili wa Savy Pops utazikwa Jumamosi Desemba 20, 2025 kwenye makaburi ya Chang’ombe, Dar es Salaam.

“Taratibu za mazishi zinaendelea, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa marehemu mtaa wa Ling’wentu Keko Juu jirani na Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (Duce), ” amesema Kaka wa marehemu.

Itakumbukwa Savy Pops enzi za uhai wake amewahi kuwa miongoni mwa mastaa wa disco Tanzania sanjari na mastaa wengine kama Bosco Cool J, Kadet Bongoman, Kokoliko na wengineo.

Savy Pops alizidi kupata umaarufu baada ya kuwa bingwa wa disco nchini Tanzania, kwenye mashindano ya kucheza disco ya Club Raha Leo Show yaliyokuwa yakiendeshwa na Masoud Masoud kupitia TBC.

Post a Comment

Previous Post Next Post