Baadhi ya Wafanyabiashara wakiwemo wasafirishaji katika Manispaa ya Shinyanga wameeleza athari za matukio yaliyotokea kuanzia tarehe 29 Oktoba na 9 Desemba.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa migogoro na vurugu ilizua hofu na kupunguza shughuli za kiuchumi katika maeneo mbalimbali na kwamba matukio hayo yameathiri mauzo, kushuka kwa wateja, na kuongezeka kwa gharama za maisha.
Aidha, wamesema kuwa amani ni kipengele muhimu kwa maendeleo ya biashara na ustawi wa jamii kwa ujumla ambapo wameshauri jamii kuepuka vurugu, na kushirikiana kuhakikisha matukio kama haya hayatokei tena.
Kwa pamoja, wamesisitiza umuhimu wa mazungumzo na mshikamano wa kijamii ili kuendeleza amani na biashara yenye tija.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment