📌 *Mitungi ya gesi 3,255 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku*
📌 *Mtungi mmoja kuuzwa kwa bei ya ruzuku TZS 17,500*.
📍 *Babati*
Kongole hizo zimetolewa leo, tarehe 04 Disemba, 2025 na wananchi wa kata ya Ayalagaya Wilaya ya Babati mkoani manyara wakati wa usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku katani hapo.
Uuzaji wa majiko hayo umeongozwa na diwani wa kata ya Ayalagaya Mheshimiwa Sabil John , mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Babati, mtendaji kata ya Ayalagaya , Afisa kutoka REA na mwakilishi wa kampuni Manjis Logistics Limited.
"Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika kutunza mazingira na afya za wananchi" amesema Mhe. Sabil.
Mhe. Sabil amesema, Lengo la mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni kuendeleza juhudi za utunzaji wa mazingira na Afya za wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu na hamasa ya kutosha na kufanya mabadiliko katika matumizi ya nishati ya kupikia.
ameongeza kuwa, Mradi huu unakuja kubadilisha mtazamo wa wananchi katika matumizi nishati ya kupikia kutoka kutumia kuni na mkaa mwingi na kuanza kutumia gesi.
Mhe. Sabil amesema, mradi huu utazambaza na kuuza mitungi ya gesi 3,255 wilaya nzima ya Babati na kata zake zote ambapo kwa mtungi mmoja mwananchi atanunua kwa bei ya ruzuku ya asilimia Hamsini (50%) ya TZS 35,000 mbayo ni sawa na TZS 17,500 tu.
" Hapo mwanzo nilikuwa nikitumia sana kuni na mkaa, ila baada ya kupata mtungi huu nimehamasika zaidi kuanza kutumia nishati safi ya kupikia na nitakuwa wa kwanza kuhamasisha wenzangu kutumia nishati safi hasa mama lishe wenzangu na wengine" alisema Bi. Barbina Koreyami mkazi wa kijiji cha Dareda Kati, kata ya Ayalagaya.
Naye, Mtendaji kata wa Ayalagaya Ndugu Onesmo Lohay ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Ayalagaya kutumia fursa hii ya upatikanaji wa mitungi kama nyenzo ya kuachana kabisa na matumizi ya nishati zisizo salama za kupikia ili kutunza afya na mazingira.
Mwisho.
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment