" ZOEZI LA KIJAMII LA UGAWAJI CHAKULA KUENDELEA MKOANI MBEYA DESEMBA 22, 2025

ZOEZI LA KIJAMII LA UGAWAJI CHAKULA KUENDELEA MKOANI MBEYA DESEMBA 22, 2025

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media

Mbeya

Desemba 22, 2025 Mkoa wa Mbeya utaendelea kushuhudia zoezi la ugawaji wa chakula kwa wananchi wenye uhitaji, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kusambaza tabasamu na kuonesha upendo kwa jamii.

Zoezi hilo litaongozwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson.

Lengo kuu la zoezi hili ni kuwapatia msaada wa chakula wananchi wenye mahitaji maalum, sambamba na kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuonesha dhamira ya kweli ya kuguswa na changamoto zinazowakabili wananchi wenye uhitaji.

Kufuatia zoezi hilo Wananchi wanahimizwa kushiriki kwa kuzingatia utulivu, nidhamu na ushirikiano ili kuhakikisha linafanyika kwa mafanikio na kwa amani.

Zoezi hili ni sehemu ya mikakati endelevu ya kijamii inayolenga kuboresha ustawi wa wananchi na kuhakikisha kuwa maendeleo yanawafikia makundi yote ya jamii.

Post a Comment

Previous Post Next Post