Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Mbeya
Mchungaji Thobias Tambikeni wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Forest ya Kwanza, mkoani Mbeya, amewataka waumini wa kanisa hilo kuonyesha msimamo thabiti katika wokovu wao na kutafuta kwa bidii ushirika wa karibu na Mungu bila kujali gharama, huku akiwahimiza kujiepusha na marafiki wabaya.
Mchungaji Tambikeni ametoa wito huo Desemba 21, 2025 wakati wa ibada ya pili iliyofanyika kanisani hapo, akisisitiza kuwa msimamo ni jambo la msingi kwa kila mtu aliyeokoka.
Amesema waumini hawapaswi kujirahisisha katika maisha yao ya kiroho, kwani kila mmoja ana thamani kubwa mbele za Mungu.
“Wasichana waliookoka thamani yao ni kubwa Msichana mwenye thamani, hata akipigiwa honi, anaonyesha thamani yake,” alisema Mchungaji Tambikeni.
Aidha, aliwahimiza vijana pamoja na watu wazima kuonyesha thamani yao katika matendo na mienendo yao ya kila siku, akisisitiza kuwa hata wazee wanapaswa kumaliza safari ya maisha yao kwa heshima na kwa kuonyesha thamani waliyonayo mbele za Mungu.
Katika mafundisho yake, Mtumishi huyo wa Mungu aliwataka waumini kujifunza kwa watu walioshinda na si kwa walioshindwa, akieleza kuwa mtu wa Mungu anapaswa kuwa na subira hata katika nyakati ambazo matokeo hayaonekani mara moja.
Pia aliwakumbusha waumini umuhimu wa kujiepusha na dhambi na kusimama imara katika eneo la Mungu kwa kusema “HAPANA” kwa mambo mabaya yanayoweza kuharibu maisha ya kiroho.
Amefafanua kuwa na msimamo hakumaanishi kuwa na kiburi, bali ni kuishi kulingana na sheria za Mungu ambazo ziko wazi, na msimamo huo ni wa lazima kwa kila muumini anayetaka kudumisha wokovu wake.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment