" Al Ahli Tripoli Waja na Ofa Nzito Kumnasa Fei Toto

Al Ahli Tripoli Waja na Ofa Nzito Kumnasa Fei Toto

 

Klabu ya Al Ahli Tripoli ya Libya inatarajiwa kutuma ofa mpya ya dola za Marekani milioni 2.5 (sawa na Shilingi bilioni 6.4) kwenda kwa Azam FC, ikiwa ni jitihada za mwisho za kumnasa kiungo nyota Fei Toto.

Hii itakuwa ofa ya tatu kutoka kwa klabu hiyo ya Libya, baada ya ofa mbili za awali kukataliwa na uongozi wa Azam FC.

Taarifa zinaeleza kuwa tayari kuna makubaliano binafsi kati ya Al Ahli Tripoli na Fei Toto, ambapo endapo dili hilo litakamilika, nyota huyo atalipwa dola 60,000 kwa mwezi (sawa na Shilingi milioni 153.6).

Sasa macho na masikio yote yanaelekezwa kwa Azam FC kuona kama safari ya Fei Toto itaendelea kusalia Chamazi au kuelekea Libya.

Post a Comment

Previous Post Next Post