" ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI





Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linapenda kujulisha kuwa limemkamata na linamshikilia Getruda Japhet Lengesela, Mkazi wa Nsalala – Mbalizi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Alikamatwa Januari 22, 2026 saa 3:40 usiku eneo la Nsalala katika Mji Mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwepo uchochezi.

Upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.

Post a Comment

Previous Post Next Post