" BURUTE SACCOS. CHAMA CHA USHIRIKA CHENYE MWELEKEO WA KIJAMII NA UONGOZI THABITI

BURUTE SACCOS. CHAMA CHA USHIRIKA CHENYE MWELEKEO WA KIJAMII NA UONGOZI THABITI

Na: Mbeki Mbeki 

Kagera.

Burute saccos ( Burute savings and credit cooperative society LTD) ni chama cha ushirika cha akiba na mikopo kinacho hudumia watumishi wa umma wa wilaya za Bukoba na Misenyi mkoani Kagera.

Chama hiki kimekuwa chombo  muhimu katika kusaidia wanachama wake kupanua uwezo wa kifedha kupitia akiba na mikopo kwa riba nafuu kwa kuzingatia kanuni na misingi ya ushirika.

Uongozi: Mwenyekiti. Mwalimu Charles Tegamaisho.

Katika shighuli mbalimbali za maendeleo ,mwenyekiti wa  BURUTE SACCOS kwasasa ni mwalimu Charles Tegamaisho,katika hafla ya utoaji misada wa vitu vya kujenga mazingira bora ya elimu kwa shule za msingi mwaka jana zenye watoto wenye mahitaji maalum, Tegamaisho alisisitiza kuwa chama sio tu chombo cha kibiashara bali pia ni mshirika wa maendeleo ya jamii.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii januari 7 mwaka huu katika manispaa ya Bukoba ,Mwenyekiti alieleza kwamba SACCOS imejipambanua kutekeleza msingi wa saba wa ushirika kujali jamii kwa vitendo kwa kutoa msaada ambao umeenda mbali zaidi ya kukopesha na kukusanya akiba ya wanachama.

Mchango wa SACCOS  chini ya uongozi wake.

 Chama chini ya uongozi wa Tegamaisho kimefanya yafuatayo: 

* Kutoa msaada wa jamii kwa shule za msingi ,madawati 340,vyandarua 205,mashuka 240,na bima za afya kwa wanafunzi ili kuboresha mazingira ya kujifunza kwa watoto wenye mahitaji maalum mkoani Kagera.

* Kuchangia katika sekta muhimu za jamii kama elimu na afya kwa kutumia mapato ya SACCOS kwa nia ya kuleta mabadiliko thabiti kwa wanachama na jamii kwa ujumla.

BURUTE  SACCOS inalenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba kwa wanachama ili kujenga uwezo wa kifedha wa kudumu,pili inalenga  kutoa mikopo  yenye mashart nafuu itakayowasaidia wanachama kuanzisha na kuimarisha biashara ,kilimo na shughuli nyingine za uzalishaji.

Aidha,SACCOS  inalenga kuinua hali ya maisha ya wanachama kwa kuwaunganisha na fursa za kiuchumi,kutoa elimu ya kifedha,na kuwajengea uwezo wa kusimamia miradi yao.

Lengo jingine ni kukuza umoja na mshikamano miongoni mwawanacha kwa misingi ya ushirika,uaminifu,na uwazi.

BURUTE SACCOS ,Pia inafanya kazi kwa lengo la kuchangia maendeleo ya jamii  ikiwemo kusaidia katika miradi ya kijamii na kiuchumi katika maeneo wanayotoka wanachama wake,hasa mkoani Kagera.


Kwaujumla malengo ya BURUTE  SACCOS yana beba dira ya uwezeshaji wa kiuchumi na ustawi wa jamii kupitia nguvu ya ushirika.

Post a Comment

Previous Post Next Post