" Dah Huzuni: Aziz K, Afiwa na Mtoto wake wa Kiume

Dah Huzuni: Aziz K, Afiwa na Mtoto wake wa Kiume

 


Klabu ya Al-Wydad Athletic ya Morocco imetoa taarifa rasmi ya rambirambi kufuatia kifo cha mtoto wa Mchezaji wao Aziz Ki. Kupitia
taarifa hiyo, uongozi wa klabu umeeleza huzuni kubwa na masikitiko makubwa kutokana na msiba huo mzito.

Katika ujumbe wao, Al-Wydad wameeleza kusimama pamoja na mchezaji
huyo katika kipindi hiki kigumu, wakimuombea yeye na familia yake wapate
faraja na subira

Klabu hiyo pia imemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu
peponi, amsamehe madhambi yake na awape familia yake nguvu, subira na utulivu wa moyo

Mwisho wa taarifa hiyo, klabu imesisitiza mshikamano wake na familia ya
marehemu, ikisisitiza kuwa msiba huo ni pigo kwa familia nzima ya Al-Wydad.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post