" DC ARUSHA AWATAKA BODABODA KUJICHANGA NUSU YA PESA YA LESENI NA YEYE ATAIJAZIA

DC ARUSHA AWATAKA BODABODA KUJICHANGA NUSU YA PESA YA LESENI NA YEYE ATAIJAZIA

 Na Seif Mangwangi, Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Modest Mkude amewataka maafisa usafirishaji wa bodaboda Jiji la Arusha kufuata Sheria za usalama barabarani ikiwemo kuwa na leseni halali ya kuwaruhusu kuendesha bodaboda zao.

Aidha amewataka kujichangisha nusu ya pesa inayotakiwa kulipia leseni ya udereva Kwa kuoridhesha majina yao na yeye atatafuta wadau Ili kujazia sehemu iliyobaki


Akizungumza Leo 14 Januari 2026, wakati akizindua mradi wa kukopeshana pikipiki chini ya chama cha waendesha bodaboda Jiji la Arusha, Mkude amesema kufuata Sheria ni jambo jema ambalo linapaswa kufuatwa na Kila anayeendesha chombo cha moto

Wakati huo huo, DC Mkude amesema operesheni kamata kamata ya pikipiki zinazokiuka Sheria za usalama barabarani ikiwemo kupiga mafataki itaendelea.

“ Operesheni kamati pikipiki itaendelea, kwanza tumegundua wanaoendesha na kufanya fujo sio wanaofanya biashara ya usafirishaji, wengi ni wahuni tu, dereva bodaboda anayejielewa hawezi kupiga mafataki huko mtaani,” amesema.

Mwenyekiti wa bodaboda Wilaya ya Arusha, Shwahibu Hamisi

Amekipongeza chama cha bodaboda Jiji la Arusha kwa kuja na mradi wa kukopeshana pikipiki, “mmefanya jambo jema sana Kikubwa muwe na nidhamu ya fedha na uadilifu, Kwa kuwa bila kufanya hivyo hawataweza kurejesha mikopo, Saccos nyingi zimekufa baada ya kukosa mambo haya,” amesema.

Amesema wakiwa makini na mradi huo wataweza kusonga mbele na kuanzisha biashara zingine ikiwemo kumiliki mabasi ya kusafirisha abiria

Aidha DC Mkude ameagiza kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha kitengo cha kuacha ukiritimba na urasimu katika kutoa leseni. 

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude

“Nawatake tu polisi mrahisishe urasimu wa kutoa leseni sio mpaka Hawa bodaboda waende mafunzo Veta, Hawa ni wafanyabiashara wataenda saa ngapi shule?, wanaotaka leseni wajiorodheshe na kupewa siku Moja wafike ukumbi wa trafiki wapewe mafunzo,” amesema.

Mwenyekiti wa umoja wa bodaboda Jiji la Arusha, Shwahibu Hamisi amesema uongozi wa umoja huo umeingia makubaliano na kampuni ya uuzaji wa bodaboda aina ya TVS kuwakopesha wanachama wao pikipiki hizo na Kwa kuanzia wamekopesha pikipiki20.

" Pikipiki hizi ni kwamba tumetumia pesa tuliyochangiwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha milioni20 ambazo tumeamua kubadilisha matumizi kutoka kuanzisha ushirika na kuamua kukopeshana bodaboda," amesema.

Amemuomba Mkuu wa Wilaya kuelekeza umoja wa bodaboda Mkoa wa Arusha kurejesha fedha za umoja huo Wilaya ya Arusha zaidi ya milioni68 Ili waweze kuzitumia kununulia pikipiki zingine na kukopesha wanachama wengi zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude akizindua mradi wa pikipiki za kukopeshana chini ya umoja wa bodaboda Wilaya ya Arusha 



Post a Comment

Previous Post Next Post