Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Ndg. Hemed Magaro, amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maendeleo kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati uliopangwa ili iweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi, hususan katika sekta za elimu na afya. Amesisitiza kuwa ucheleweshaji wa miradi huwakosesha wananchi fursa muhimu za huduma za msingi.Ndg. Magaro alitoa maelekezo hayo tarehe 07 Januari, 2026 alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata za Mandawa na Lihimalyao wilayani Kilwa. Katika ziara hiyo, alikagua ujenzi wa shule mpya ya Elimu ya Awali na Msingi unaojengwa katika eneo la Sekondari ya Mpunyule, mradi uliogharimu Shilingi 314,000,000 kutoka mradi wa BOOST, wenye lengo la kuongeza upatikanaji wa elimu na kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.Aidha, Mkurugenzi Mtendaji alikagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari katika Kijiji cha Kisongo, Kata ya Lihimalyao, mradi uliogharimu Shilingi 547,736,870. Mradi huo unalenga kuongeza fursa za elimu ya sekondari kwa wanafunzi wa eneo hilo pamoja na kata jirani, hivyo kupunguza umbali wa wanafunzi kufuata huduma ya elimu.Pia, Ndg. Magaro alitembelea mradi wa umaliziaji wa Zahanati ya Kijiji cha Mkondandaji, Kata ya Mandawa, uliogharimu Shilingi 62,324,120, na kusisitiza umuhimu wa kukamilishwa kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na huduma za afya. Akihitimisha ziara yake, aliwataka wasimamizi wa miradi na wakandarasi kuzingatia ubora, thamani ya fedha na ratiba ya utekelezaji, huku akiahidi kuwa Halmashauri itaendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha miradi inaleta tija iliyokusudiwa kwa wananchi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254










Post a Comment