Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMbeyaLeo Januari 7, 2026, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, ametembelea na kukagua mifereji ya kupitishia maji katika Kata ya Itezi, Jijini Mbeya.Dkt. Tulia amefanya ukaguzi huo kwa lengo la kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto za upitishaji wa maji, ili kuyawezesha kupita kwa urahisi na kufuata mkondo wake wa asili. Hatua hiyo inalenga kupunguza adha wanayokumbana nayo wananchi wa eneo hilo, hususan wakati wa mvua zinazoendelea kunyesha.Amesisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu ya mifereji ili kujiepusha na majanga ya mafuriko yanayoweza kujitokeza kutokana na miundombinu isiyo rafiki, huku akieleza kuwa hatua za mapema ni muhimu katika kulinda maisha na mali za wananchi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment