Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMbeya Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, ametembelea na kukagua daraja la Tonya lililoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.Daraja hilo lipo kwenye barabara inayounganisha mitaa ya Tonya na Shewa (Stoy Road) katika Kata ya Mwakibete, na limekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi kufanikisha shughuli zao za kila siku.Katika ziara hiyo, Dkt. Tulia alisikiliza kwa makini changamoto ya barabara hiyo kutopitika, hali inayowaathiri wananchi pamoja na wanafunzi wanaotumia njia hiyo kuelekea shuleni. Kufuatia changamoto hiyo, aliagiza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kufika haraka eneo hilo na kuchukua hatua za dharura ili kurejesha mawasiliano na usalama wa Wananchi.Aidha, Dkt. Tulia amewapa pole Wananchi wa eneo hilo kwa usumbufu unaosababishwa na uharibifu wa daraja hilo, huku akitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kuzingatia mipango bora ya ujenzi. Aliwasihi wananchi kujiepusha na kujenga katika maeneo hatarishi hasa wakati wa kiangazi, ili kuepuka athari kubwa pindi mvua zinaponyesha.Ziara hiyo inaonesha dhamira ya viongozi kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi, hususan katika miundombinu inayogusa maisha ya kila siku ya jamii.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment