Na Mwandishi wetu, Misalaba Media Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Mbinga Mji, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Suzo Xavery Komba, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo tofauti ya Halmashauri, ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi hiyo.Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Suzo Xavery Komba amekagua ubora wa ujenzi pamoja na hatua za utekelezaji wa miradi, huku akisisitiza umuhimu wa thamani ya fedha kuonekana katika miradi yote inayotekelezwa. Aidha, ametoa maelekezo kwa wataalam wa Halmashauri kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati, viwango vya ujenzi vinazingatiwa na wananchi wanapata huduma bora na endelevu.Vilevile, Mheshimiwa Suzo Xavery Komba amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na wataalam kwa usimamizi mzuri na wa karibu wa miradi ya maendeleo.Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati ya Tukuzi, ujenzi wa Zahanati ya Kihuka, ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Nyerere, ukarabati wa Shule ya Msingi Mbinga pamoja na ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Lusonga.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment