" ELAF YATOA WITO KWA VIONGOZI WA SERIKALI KUHESHIMU MAAMUZI YANAYOTOLEWA NA MAHAKAMA

ELAF YATOA WITO KWA VIONGOZI WA SERIKALI KUHESHIMU MAAMUZI YANAYOTOLEWA NA MAHAKAMA

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media‎Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Legal and Human Rights Centre (ELAF) kimeitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na watumishi wake kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Katiba ya nchi, sheria zilizopo pamoja na kuheshimu maamuzi ya mahakama.‎Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 26, 2026 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa ELAF, Wakili Khamisi Mohamed,amesema kuna umuhimu mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa sheria kwa umakini ili kuzuia vitendo vya kiholela vinavyokiuka haki za raia.‎Wakili Khamisi amesisitiza kuwa viongozi au watumishi wa umma wanaokiuka amri na maamuzi ya mahakama hawapaswi kuvumiliwa, akieleza kuwa tabia hiyo inadhoofisha misingi ya utawala wa sheria, haki na demokrasia nchini.‎“Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa watumishi wake wote wanatii Katiba na sheria za nchi, pamoja na kuheshimu maamuzi ya mahakama. Kushindwa kufanya hivyo ni kuvunja misingi ya haki na demokrasia,” amesema Wakili Khamisi.‎Kauli hiyo imetolewa kufuatia tukio lililoripotiwa hivi karibuni katika eneo la Mbezi Msakuzi jijini Dar es Salaam, ambapo nyumba ya raia mmoja, Pili Kafuye, ilidaiwa kubomolewa kwa nguvu na mali zake kutupwa nje, hali iliyoibua maswali kuhusu ulinzi wa haki za wananchi hususan katika masuala ya ardhi na makazi.‎Kufuatia tukio hilo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, alitoa agizo la kuchukuliwa hatua za haraka kurekebisha hali hiyo pamoja na kubaini watu waliohusika na uvunjifu wa sheria ili wachukuliwe hatua za kisheria.‎ELAF imesema itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa sakata hilo na kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika wa vitendo vya ukiukwaji wa haki, huku ikisisitiza umuhimu wa uwajibikaji kwa wote wanaohusika katika kulinda utawala wa sheria nchini.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post